Iyanya akataa ombi la ndoa kutoka kwa muigizaji mrembo Yvonne Nelson
Muigizaj mrembo kutoka Ghana "Yvonne Nelson, ameachana na muimbaji
Iyanya mara tu baada ya kumpa story kuhusu ndoa na kukataliwa.
Yvone alitaka kupeleka mahusiano yake na Iyanya katika levo nyingine,
lakini hawakuwa katika ukurasa mmoja,Ripoti kutoka kwa mtu wa karibu wa
Yvonne zinadai kuwa muigizaji huyo alimuambia Iyanya kuwa anataka ndoa
na kumfanya awe mumewe rasmi, lakini jinsi alivyoichukulia ilimshtua
sana,maana Iyanya anahisi ni mapema sana kuongelea ishu hiyo.
mtu huyo wa karibu aliendelea kuelezea kwanini mwanadada huyo aliumia baada ya kujibiwa hivyo..
"wakati msichana akikuambia kuwa anakupenda na anataka mahusiano hayo
yasonge mbele na kuaza maisha rasmi na wewe na hata kuwa na wewe kama
mume wake na ukamkatalia, hiyo ni mbaya sana, ni kama kusema, mchezo ndo
umeishia hapo" alisema mtu huyo