ACHEL ASAKA BWANA WA ‘KUMBONJI’ NAYE KENYA
MWANAMUZIKI Winfrida Josephat ‘Rachel’ juzikati aliwashangaza watu baada ya kudai kwamba siku hiyo baada ya shoo yao akiwa na Kundi la Kigoma All Stars mjini Nairobi alikuwa akitafuta bwana wa kumpa kampani usiku bila mafanikio.
Rachel akijiachia na shabiki wake stejini.
Mtandao mmoja wa Kenya wa Standard Digital News uliandika kuwa, siku
hiyo baada ya shoo akiwa anazungumza na mapaparazi wa huko binti huyo
alisema alikuwa akitaka mtu wa ‘kujivinjari naye’ lakini akafedheheka
kwa kumkosa yule wa kumpa furaha ya kimahaba.
Rachel akiwa kazini.
Gazeti moja la habari la Global Publisher lilimtafuta Rachel kupitia simu yake ya mkononi kuzungumzia hilo na alipopatikana alisema:“Mimi kuongea hivyo si kitu cha ajabu kiasi cha kuifanya mitandao ya Kenya inicharukie. Kwani kuna ubaya gani kusema natafuta mtu wa kuniridhisha? Ile ni mbinu tu ya kuwateka mashabiki.”
No comments:
Post a Comment