Baby Madaha adai maneno ya watu yaliyosabisha aingie kwenye Mapenzi na Meneja wake (Mkenya)
Kama ningekuwa Soud Brown aka Gossip Cop basi ningetumia msemo wa U
Head!!!Hivi sasa sio siri tena kwani Baby Madaha ameamua kukiri na
kuweka wazi kuhusu uhusiano wa kimapenzi na bosi wa Candy n Candy 'Joe
Kariuki'
Msanii huyo wa filamu na muziki hapa nchini Tanzania Baby Joseph
Madaha,ameimbia Global Publishers kuwa mwanzo yeye na Meneja wake
hawakuwa na uhusiano wa kimapenzi toka aanze kusimamiwa kazi zake,lakini
kutokana na maneno ya watu kumzushia ambacho kitu akipo basi ndio
kilichompelekea aingie kweli kwenye Mapenzi na Meneja wake.
' “Kusema kweli
huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi lakini abadani
sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na uhusiano naye ila
porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo natamani niamie Kenya
ili tuwe karibu wakati wote,”alisema Baby Madaha.
Aliongeza kuwa kikubwa kilichompelekea kuwa naye ni kutokana na upendo wake wa kweli alionao kwake siyo kutokana na suala la mkwanja kama wengi wanavyodhani.
Aliongeza kuwa kikubwa kilichompelekea kuwa naye ni kutokana na upendo wake wa kweli alionao kwake siyo kutokana na suala la mkwanja kama wengi wanavyodhani.
As copyrighted from Dj Fety
No comments:
Post a Comment