ANG'ATWA NA NYOKA SEHEMU NYETI AKIWA MSALANI
Mwanaume huyo mwenye umri wa mika 35, aliwaeleza madaktari kuwa aligundua kuwa ameng'atwa na nyoka baada ya kusikia muwasho sehemu zake nyeti ndipo alipoangalia chini na kumuona nyoka mdogo akikimbia.
Madaktari walidai kuwa jamaa huyo alikuwa katika hali nzuri mbali na wasiwasi alioupata baada ya kung'atwa na nyoka huyo ambaye hakuwa na sumu. Daktari mwingine alisema: "hii ni mara yangu ya kwanza kuona mtu ameng'atwa na nyoka sehemu hiyo nyeti.
Kwa bahati nzuri kila kipimo kinaonekana kipo vizuri na mgonjwa anaendelea vizuri."
Kama mwanaume huyo angeng'atwa na nyoka wenye sumu kali kama koboko basi mambo yangekuwa yameharibika kabisa.