MAKOSA 10 WANAWAKE HUYAFANYA WAKIWA FARAGHA
Uhusiano wa kimapenzi una wigo mpana. Kuna mambo mengi ambayo yakifanywa huufanya mwili uwe na afya. Hata hivyo, suala la faragha halipaswi kusahaulika, kwa maana ni chachandu madhubuti.
Tendo la faragha lina nguvu sana katika kuuweka hai uhusiano. Wapo watu ambao picha zilikuwa haziendi katika maisha ya kawaida lakini kila wakikutana kitandani, kila mmoja alimvulia kofia mwenzake.
Hii ina maana kuwa inawezekana mwenzi wako akawa dhaifu katika maeneo mengine lakini ‘maujuzi’ yake faragha, yakakufanya uwe mtulivu kwake.
Vivyo hivyo, nawe hakikisha unampatia mwezi wako katika eneo fulani ili hata akikufanyia visa, basi uwe na ukurasa wako ambao akiufikia ni lazima akuvulie kofia. Faragha ni uwanja huru ambao ambao hudhaniwa ni mgumu lakini ni rahisi sana.
Haihitaji msuli mkubwa wala nguvu kama za samba. Usidanganyike kwenda kutumia madawa ya kuongeza nguvu wala kwenda kwa waganga eti ndiyo wakuboreshee mvuto wako. Tuliza kichwa, soma kitendo chenyewe halafu hakikisha hufanyi makosa.
Katika makosa mengi ambayo wanawake huyafanya wakiwa faragha, ndani ya mada hii, nimeyaunganisha na kuyafanya yasomeke 10. Nikuhakikishie kuwa ukiyaepuka na kufuata mwongozo sahihi, utakuwa bora sana.
Mambo mengi hayahitaji taaluma, ni suala la kuushirikisha ubongo ili uamue kinachotakiwa. Mathalan; kuzungumza na mwenzi wako kumuuliza nini umfanyie ili afurahie tendo au kumwelewesha cha kufanya aweze kukupatia, haihitaji maarifa mengi au uwezo wa juu kiakili.
Kujifanya unajua sana husababisha wengi kuchemka. Achana na tabia ya kuhisi wewe umekamilika na kujidanganya kwamba unafahamu kila kinachotakiwa katika uwanja mahsusi wa faragha. Inakugharimu kiasi gani kuzungumza naye ili akujuze mahali hisia zake zilipolalia?
Yupo mwanamke ambaye tangu anazaliwa mpaka anakua, amekariri kwamba ukiwa faragha dawa ni kuzungusha ‘bakuli’ mwanzo mwisho. Matokeo yake, anakutana na mwenzi wake, badala ya kusoma mahitaji yake, yeye akili, nguvu na ujuzi wake wote anauelekeza katika nyonga tu. Mauno mtindo mmoja.
Hajui kwamba pengine mwenzi wake hapendi purukushani za kupanda na kushuka. Inapotokea wewe ni mtaalamu wa kucheza juu ya msumari (wana wa unyago mnaelewa), dakika 90 hushushi mzigo chini, ukidhani unamfurahisha, kumbe unageuka kero kwa mwezio.
Inaweza kutokea umekariri kuwa ukiwa katika utekelezaji wa sanaa ya faragha lazima uporomoshe mayowe. Japo ni nzuri katika kupata mrejesho (feedback) wa tendo lenyewe lakini si ajabu mwenzako hafurahii hilo. Zungumza naye tafadhali.
Hekima za tendo zinakataa ububu, lazima muwe mnaambiana mara kwa mara. Kama siku hajakutendea haki, mweleze waziwazi kwamba hajakufikisha. Ukimwacha afanye anachotaka na anachojisikia yeye, mwishowe haitakuwa na msisimko kwako.
Tengeneza utofauti wa makutano ya mbuzi na binadamu. Maana beberu huwa hajui maana ya kumwandaa jike. Anapojisikia kupanda anafanya hivyo na anapotosheka anashuka. Wewe na mwenzi wako hamna budi kuwa na nidhamu. Hisia ziheshimiwe.
Ikiwa mtatenda kwa makubaliano, kila mmoja akifuata maelekezo ya mwenzi wake, akitilia mkazo yale maeneo ambayo yametajwa katika mazungumzo kwamba ndiyo huleta raha, basi raha huwa raha kweli. Zingatia mambo 10 yafuatayo;Tuungane katika sehemu ya pili