JIFUNZE
Mpendwa,
Siku moja punda wa mkulima
alianguka ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga kelele kinyonge kwa
masaa kadhaa wakati mkulima akijaribu kufikiri nini cha kufanya.
Hatimaye, aliamua kwakuwa
punda wake alikuwa mzee, na pia kisima hicho kilihitaji kufunikwa juu,
Akaona hapakuwa na haja ya kumtoa.
Akaita majirani zake wote waje
kumsaidia. Wao wote wakachukua makoleo na kuanza kuchota taka kwa koleo
na kuzitupia ndani ya kisima.
Mara ya kwanza, punda aligundua nini
kilikuwa kinatokea akapiga kelele kwa nguvu. Basi, ikawashanganza wale
watu punda aliponyamaza ghafla!
Baada ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho kisima. Huyo mkulima
alishangazwa na kile alichokiona. Kwamba kila koleo la taka
lililorushwa juu ya mgongo wa punda, punda alikuwa akifanya kitu cha
kushangaza. Alikuwa akijitikisa ili taka zimwagike chini huku akipiga
hatua moja kuja juu.
Kadri mkulima na majirani walivyoendelea
kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda yule, alizidi kutikisa mgongo wake
na kupiga hatua moja kuja juu. Muda mfupi baadae, kila mtu alishangaa
jinsi punda alivyozidi kutokeza ndani ya kisima na kuja juu.
FUNZO:
Maisha
yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili utoke nje ya kisima wahitaji
kujitikisa na kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo ulilonalo, ni jiwe la
kukuwezesha kukanyaga na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka nje ya
kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya kupiga hatua moja kuja juu bila
kuacha na kutokata tamaa kamwe. Tikisa itikisa uchafu mbali na kuchukua
hatua kuja juu.
Kumbuka kanuni 5 rahisi ili uwe na furaha:
1. Weka huru moyo wako mbali na chuki - Samehe.
2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi - Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.
3.Tosheka / rizika na ulichonacho.
4. Toa zaidi.
5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini zaidi kutoka kwako mwenyewe.
Una uchaguzi wa aina mbili ...
i) Tabasamu na funga ujumbe huu,
ii) au tuma ujumbe huu kwa mtu mwingine ili ashiriki somo hili
Imetumwa na: Dr. Emeria A. Mugonzibwa - Mwanga.
No comments:
Post a Comment