copyrighted from global publishers
RAY C AHAHA KUONDOA MINYAMA UZEMBE, ABATIZWA KWA MAJI MENGI.

Hakika
sexy lady kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amepona na sasa
anahaha kukata minyama uzembe baada ya kuachana na matumizi ya madawa ya
kulevya ‘unga’.

Ray
C au Kiuno Bila Mfupa, juzikati alitupia picha kwenye ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii wa Instagram zikimuonesha akiwa ‘bize gym’ akifanya
mazoezi makali kupunguza unene akijiandaa kurejea rasmi kwenye gemu.
Picha hizo zinamuonesha akikimbia kwenye mashine maalum ya
kukimbilia, akifanya mazoezi ya viungo na nyingine akifanya mazoezi ya
kukata tumbo ambapo mashabiki wake kwa asilimia kubwa walimpongeza kwa
hatua hiyo.

“Kiuno Bila Mfupa umetishaaa…sasa umerudi enzi zile…bora ulivyoamua kufanya mazoezi,” yalisomeka sehemu ya maoni hayo.
Baada ya kupona na kuacha madawa ya kulevya kwa msaada wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete baada ya kutolewa
kwenye magazeti ya Global akiwa hoi, sasa anasubiriwa kwa shauku na
mashabiki wake wanaotamani kumuona stejini kwa mara nyingine.

Wakati
gazeti hili linakwenda mitamboni lilipokea ‘nyiuzi’ kuwa Septemba 29,
mwaka huu (Alhamisi) iliyopita, Ray C alibatizwa kwa maji mengi katika
Kanisa la Sloam lililopo Bunju, Dar.tunakusubiri sana dada tumemiss sauti yako.
No comments:
Post a Comment