MAKOSA 10 WANAWAKE HUYAFANYA WAKIWA FARAGHA
Kitanda
kina kanuni zake. Kuna makosa mengi hufanywa na wanawake, vilevile yapo
ambayo wanaume huyafanya. Si sawa kuyaacha yaendelee kuwepo kwa sababu
faragha ni hatua muhimu katika ukamilishaji wa kitu kinachoitwa penzi.
Uhusiano wa kimapenzi una wigo mpana. Kuna mambo mengi ambayo
yakifanywa huufanya mwili uwe na afya. Hata hivyo, suala la faragha
halipaswi kusahaulika, kwa maana ni chachandu madhubuti.
Tendo
la faragha lina nguvu sana katika kuuweka hai uhusiano. Wapo watu ambao
picha zilikuwa haziendi katika maisha ya kawaida lakini kila wakikutana
kitandani, kila mmoja alimvulia kofia mwenzake.
Hii ina maana kuwa inawezekana mwenzi wako akawa dhaifu katika maeneo
mengine lakini ‘maujuzi’ yake faragha, yakakufanya uwe mtulivu kwake.
Vivyo hivyo, nawe hakikisha unampatia mwezi wako katika eneo fulani
ili hata akikufanyia visa, basi uwe na ukurasa wako ambao akiufikia ni
lazima akuvulie kofia. Faragha ni uwanja huru ambao ambao hudhaniwa ni
mgumu lakini ni rahisi sana.
Haihitaji msuli mkubwa wala nguvu kama za samba. Usidanganyike kwenda
kutumia madawa ya kuongeza nguvu wala kwenda kwa waganga eti ndiyo
wakuboreshee mvuto wako. Tuliza kichwa, soma kitendo chenyewe halafu
hakikisha hufanyi makosa.
Katika makosa mengi ambayo wanawake huyafanya wakiwa faragha, ndani
ya mada hii, nimeyaunganisha na kuyafanya yasomeke 10. Nikuhakikishie
kuwa ukiyaepuka na kufuata mwongozo sahihi, utakuwa bora sana.
Mambo mengi hayahitaji taaluma, ni suala la kuushirikisha ubongo ili
uamue kinachotakiwa. Mathalan; kuzungumza na mwenzi wako kumuuliza nini
umfanyie ili afurahie tendo au kumwelewesha cha kufanya aweze kukupatia,
haihitaji maarifa mengi au uwezo wa juu kiakili.
Kujifanya unajua
sana husababisha wengi kuchemka. Achana na tabia ya kuhisi wewe
umekamilika na kujidanganya kwamba unafahamu kila kinachotakiwa katika
uwanja mahsusi wa faragha. Inakugharimu kiasi gani kuzungumza naye ili
akujuze mahali hisia zake zilipolalia?
Yupo mwanamke ambaye tangu anazaliwa mpaka anakua, amekariri kwamba
ukiwa faragha dawa ni kuzungusha ‘bakuli’ mwanzo mwisho. Matokeo yake,
anakutana na mwenzi wake, badala ya kusoma mahitaji yake, yeye akili,
nguvu na ujuzi wake wote anauelekeza katika nyonga tu. Mauno mtindo
mmoja.
Hajui kwamba pengine mwenzi wake hapendi purukushani za kupanda na
kushuka. Inapotokea wewe ni mtaalamu wa kucheza juu ya msumari (wana wa
unyago mnaelewa), dakika 90 hushushi mzigo chini, ukidhani
unamfurahisha, kumbe unageuka kero kwa mwezio.
Inaweza kutokea umekariri kuwa ukiwa katika utekelezaji wa sanaa ya
faragha lazima uporomoshe mayowe. Japo ni nzuri katika kupata mrejesho
(feedback) wa tendo lenyewe lakini si ajabu mwenzako hafurahii hilo.
Zungumza naye tafadhali.
Hekima za tendo zinakataa ububu, lazima muwe mnaambiana mara kwa mara.
Kama siku hajakutendea haki, mweleze waziwazi kwamba hajakufikisha.
Ukimwacha afanye anachotaka na anachojisikia yeye, mwishowe haitakuwa na
msisimko kwako.
Tengeneza utofauti wa makutano ya mbuzi na binadamu. Maana beberu huwa
hajui maana ya kumwandaa jike. Anapojisikia kupanda anafanya hivyo na
anapotosheka anashuka. Wewe na mwenzi wako hamna budi kuwa na nidhamu.
Hisia ziheshimiwe.
Ikiwa mtatenda kwa makubaliano, kila mmoja akifuata maelekezo ya mwenzi
wake, akitilia mkazo yale maeneo ambayo yametajwa katika mazungumzo
kwamba ndiyo huleta raha, basi raha huwa raha kweli. Zingatia mambo 10
yafuatayo;Tuungane katika sehemu ya pili