look around you

look around you
mysef

Saturday, August 31, 2013

MZEE MAGALI HAKUMBUKI KACHEZA MUVY NGAPI?

ETI MZEE MAGALI HAKUMBUKI IDADI YA FILAMU ALIZOCHEZA

KATIKA hali iliyoonesha kushangaza wengi, hivi karibuni staa wa sinema za Kibongo, Charles Magali ‘Mzee Magali’ alisema eti hakumbuki idadi ya filamu alizoigiza wala majina yake.
Mzee Magali aliibua kituko hicho wakati akibadili nguo kuingia kurekodi filamu mpya ya Pasuko la Moyo ya Quick Promotions ambayo itaingia barabarani Septemba 17, mwaka huu.
“Mimi kazi yangu ni kukamua tu, sijui nimeshacheza filamu ngapi, sikumbuki hata majina yake, wanajua wenye filamu, ninayoijua ni hii ya Pasuko la Moyo kwa sababu ni mpya, kwa hiyo kuanzia sasa naanza kuzishika kichwani,” alisema mzee huyo kwa sauti kali

No comments:

Post a Comment