look around you

look around you
mysef

Tuesday, July 16, 2013

MSANII SHILOLE KAMA KAWA............

MSANII ASIYE ISHIWA MATUKIO ADADA VUA KUHUSIANA NA PICHA ZAKE ZA INSTAGRAM ZIKIMUONYESHA AKIWA AMEVAA TAULO

  
Siku kadhaa tangu alipo-post picha akiwa amevaa taulo, huku mitandao ikiripoti kuwa alikuwa supermarket akiwa nchini Marekani, Shilole amekanusha kutembea na taulo supermarket na kusema kuwa alikuwa akiogelea katika swiming pool iliyoko nyuma ya hoteli aliyofikia.
"Ile ilikuwa nipo swiming pool sawa, hoteli niliyokuwa ninakaa ilikuwa na swiming pool pembeni,  unajua miji ya wenzetu bana, imekaa yaaani yaaani ukitizama hivi mtu anaweza akasema, ina maduka meengi, halafu hoteli yetu sisi kubwa chini kuna swimming pool kwa nyuma, kwa hiyo mi nilikuwepo kule nyuma pale swiming pool naoga, nimetoka kuoga ni Masanja ndio akanipiga picha.
kwahiyo hiyo picha mi nimeitupia tu instagram, kwamba hakuna mtu ambae anaweza kama, kama huku Tanzania mtu labda kusema unaweza ukasimamama kutoka hapa, umetoka swmming pool si iko hapa, mtu labda akaanza kukushangaa.
Nimejaribu kuona nimeona wenzetu huko wa Africa, hawana taimu na mtu hata uvae kichupi hana taimu na wewe, yaani kila mtu anafanya  mambo yake, kwasababu hata sasa hivi kule ni kipindi cha summer, kwahiyo watu wanavaa hivi, kwahiyo mi nilivyokua nimevaa vile sio kwamba nilikuwa nimevaa naenda supermarket, nilikuwa naenda swimming pool." 
HUO NDIO UFAFANUZI WAKE

No comments:

Post a Comment