Lina Medina mtoto wa miaka mitano (5)....wa Ticrapo
nchini Peru mwaka 1939 alizaa mtoto wa kiume na akaitwa Gerardo.Wazazi
wake walidhani ana uvimbe tumboni alipopelekwa hospitali kupimwa akakutwa na
ujauzito wa miezi saba.
Lina alikuwa mtoto wa kawaida kama watoto wengine tu
lakini kwa mujibu wa baba yake alishaanza kupata periods zake mapema.Jina la
mtoto wake Gerardo lilitokana na jina la daktari
aliyemuhudumia.
Ishu ya Lina iliwasumbua sana madaktari
imewezekanaje yeye kupata mtoto?baba wa mtoto?alibakwa?
Baba wa Lina alifunguliwa mashtaka ya kuhusishwa
kumbaka lakini alikuja kuachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.Lina
mwenyewe hakuwahi kusema alipataje huo ujauzito.Baba wa mtoto wa Lina hakuwahi
kujulikana na hata namna ambavyo mtoto huyo wa miaka mitano alivyoweza kupata
ujauzito.
Kwa sababu ni jambo lisilo la kawaida madaktari
walijaribu kufanya tafiti za kila aina.Baada ya research iligundulika Lina
alikuwa na tatizo la hormone disorder na madaktari walitaka akae hospital kwa
uchunguzi zaidi wa kisayansi lakini familia yake ilikataa.Wakamchukua mtoto wao
na kumlea yeye na mtoto wake pamoja na mdogo wake.Mtoto wa Lina alilelewa kama
mdogo wake na hata akikuwa alijua Lina ni dada yake mpaka alipotimiza miaka 10
ndio alijua kuwa ni mama yake.
Pichani lina akiwa na mwanae
Kwenye maisha yake ya usichana alifanya kazi ya
usecretary kwenye Lima clinic.Hii ni clinic ya Dr. Lozada aliyejitolea
kumsomesha yeye na pia kumsommesha mtoto wake high school.
Alikuja kuolewa na kupata mtoto wake mwingine mwaka
1972 akiwa na miaka 39.Mwaka 2002 waandishi wengi wa habari walimfata kwa
mahojiano wakiwemo Reuters lakini aliwatolea nje kuongelea chochote kuhusu
maisha yake.
Mwaka 1979 mtoto wa Lina Gerardo alifariki dunia
akiwa na miaka 40 kwa matatizo ya bone marrow.
Na inasemekana Lina Medina bado yu hai.
No comments:
Post a Comment