MAMA ALIYEKAA JUU YA PAA KUPINGA NYUMBA YAKE KUUZWA NA BANK!!
Huyu mama
alikaa juu ya paa kwa siku tatu tangu jumamosi kupinga nyumba yao kuchukuliwa na
bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu alipochukua mkopo bank miaka mingi iliyopita
na kushindwa kulipa mkopo huo.
Kwa mujibu wa
maelezo yake kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali
zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa alikopa
ml 240 wameuza nyumba zake 2 na mabasi mawili.Wenyewe wanachodai katika hilo
deni imebaki tsh ngapi na wao watoe?kama nyumba iuzwe watoe deni la bank na hela
inayobaki wabaki nayo wao.
Nyumba ipo
mbezi Tangi bovu na inaeneo kubwa sana mama anasema hata akiuza si chini ya ml
500 iweje atolewe kwa ml 240?wakati mdaiwa nyumba zake mbili zimeshachukuliwa na
mabasi mawili yale makubwa ya safari za mikoani.Hiyo ml 240 haijatimia tu?na
kama bado kiasi gani kimebaki?
Ndani ya
nyumba vitu walishachukua hao watu wa auction mart ndani kweupe.Na wakati haya yakiendelea
hakukuwa na amri yoyote iliyotoka mahakamani wala hawakuwa na kibali cha
mahakama.
Gea alimfata
huko huko juu kumsikiliza na tumemsikia leo kwenye heka heka.Kesho pia
itaendelea.
Hapa mabaunsa
wakimfukuza
Wamemshika
Wamempa kanga
nyingine 2 ajifunge maana hakuwa na nguo zaidi ya hiyo kanga
moja.
Eneo la nje
kulivyokuwa
Nje ya geti
la hiyo nyumba
Chumba cha
habari cha clouds fm kimeenda kufatilia hapo bank ya Tanzania Investment
bank(TIB)kujua kulikoni??
Maana wakati
haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba imeshauzwa.Inauzwaje na shauri
lipo mahakamani?Na jana mume wa huyu mama alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku
ya kesi kuendelea kusikilizwa.
Na mumewe
alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao
virudishwe.
copywright by dina marios
No comments:
Post a Comment